Kilimo Cha Kabeji


 

 

Aina ya Kabeji


  • Kabeji inayokuwa mapema
  • Kabeji inayokuwa taratibu

Aina za Mbegu

o   Drumhead variety


Ina vichwa vikubwa sana na mara nyingi ni bapa juu. Ipo katika aina za kabeji zinazo kuwa taratibu kwasababu inachukuwa siku 110 mpaka siku 120. 

Ikikuwa ina kichwa chenye uzito wa kilo 2 mpaka kilo 2.5. Upasuka kwa uwepesi.

o   Copenhagen

Ina vichwa vya mviringo na ipo katika aina za kabeji zinazo kuwa mapema ikitumia siku 90 mpaka siku 100, ila upasuka kwa uwepesi.

o   Ox heart

Huwa na vichwa vidogo vyenye umbile kama moyo. 

Ipo katika aina za kabeji zinazo kuwa mapema ikitumia siku 90 mpaka 100, haipasuki kwa uwepesi na inaradha nzuri.

o   Early Jersey

Ina vichwa mfano wa koni vyenye ukubwa wa kati. Ipo katika aina za kabeji zinazo kuwa mapema ikitumia siku 90 mpaka 100. 

Zenye vichwa vyenye uzito wa kilo 1.5 mpaka kilo 2.

o   Glory of Enkhuizen

Ina vichwa vya mviringo na ipo katika aina za kabeji zinazo kuwa kwa taratibu ikitumia siku 110 mpaka 120 baada ya kutolewa kwenye kitaru.
  • Groria   F1 Hybrid

Gloria F1 Hybrid
Ukuwa ndani ya siku 80 mpaka siku 90 baada ya kupandwa kutoka kwenye kitaru. 

Huwa na vichwa vizuri vya mviringo vyenye rangi ya blue kijani, huwa na uzito wa kilo 2.5 mpaka kilo 4. 

Huwa nauweza wa kuvumilia hali ya hewa tofauti tofauti. Huweza vumilia joto na ugonjwa wa Fusarium yellow.

Idadi ya Mbegu

Gram 200 mpaka 250 kwa hekta.

Hali ya Hewa

  • Nyuzi joto 15-200C.
  • Juu ya 250C hupunguza uzalishaji.

Sifa za Udongo

  • Mdongo mzuri usio kuwa na maji ya kutuhama.
  • Udongo wa kichanga mzito au tifutifu au hata wa mfinyanzi.
  • Udongo wenye PH ya 6.5 – 6.8
  • Uweza vumilia udongo wenye chumvi chumvi.

Huoteshaji

Kabeji huoteshwa kwa mbegu. Uweza pandwa moja kwa moja shambani au kwenye kitaru kwanza halafu baadae kuamishiwa shambani.

Miche


      Miche iko tayari kuamishiwa shambani kutoka kwenye kitaru baada ya wiki 4 mpaka wiki 6 baada ya kupandwa, 

    kawaida wakati  huu miche huwa na urefu wa Sm 15 mpaka Sm 20.

          
         Kabila miche kuamishwa inabidi kukomazwa kwanza.

Mbegu


·         Ikipandwa kwa mbegu shambani baada ya wiki 3 mpaka wiki 4 inaitaji kupunguziwa kama ipo zaidi ya mche moja kwa shimo na kubaki mche moja kwa shimo

·         
      Ila pia wakati huu sehemu ambazo mbegu hazikuota basi miche iliyoamishwa toka sehemu iliyozidi huwekwa sehemu hizi kuziba nafasi iliyokuwa imebaki.

Red Cabbage aina Kifaru F1

Hatua za Upandaji

Huwa pandwa katika mistari na hupewa nafasi kuendana na aina ya kabeji.

  • Nafasi kati ya mstari na mstari uwa Sm 50 mpaka Sm 90 na nafasi kati ya mche na mche uwa Sm 25 mpaka Sm 60. Kwa nafasi hizi shamba la hekta moja huwa na miche 22,000 mpaka 80,000. 
       Mfano: Ox-heart huwa na Sm 50 x Sm 40 (kati ya mstari X kati ya miche), Drumhead huwa na Sm 75 x Sm 60.
  • Katika uzalishaji wa kabaji, nafasi kubwa huacha kwa ajili ya uzalishaji wa kabeji ya vichwa vikubwa na nafasi ndogo kwa kabeji ya vichwa vidogo.

Matumizi ya Mbolea

  • Kabeji huitaji virutubisho vingagi wakati wa ukuwaji wake, kama kilo 60 ya N (Nitrogen), kilo 60 ya P (Phosphorus) na kilo 150 ya K (Potassium) kwa heckta wakati wakupanda kutoka kwenye kitaru na baadae mbolea ya juu ya N (Nitrogen) wakati wa kukuwa.
  • Pia mbolea ya K (Potassium) inaweza tumika kwa 50% wakati wakupanda kutoka kwennye kitaru.
  • Mbolea ya juu iwekwe kati ya wiki 2 mpaka 4, wiki 4 mpaka 6 na wiki 8 mpaka 10 baada ya kutoa kwenye kitaru.
  • Mbolea iwekwe kwa mduara kwa umbali wa Sm 10 mpaka 15 kutoka kwenye mme.

Matumizi ya Maji

  • Kabeji inaitaji maji mengi ya kutosha baada ya kupanda kutoka kwenye kitaru. Udongo mubichi (wenye maji) ni muhimu wakati wa kupanda shambani kutoka kwenye kitaru.
  • Kwa kuzalisha wa kabeji yenye ubora, umwagiliziaji niwa lazima kiwango cha chini sana kiwe mara mbili kwa wiki, ikitegemea hali ya hewa na aina ya udongo. 
  • Upungufu wa maji uchelewesha utengenezaji wa kichwa cha kabeji na usababisha kuwa na vichwa vidogo.
  • Inabidi kumwagilizia maji ya kutosha mpaka wakati wa kuvuna.

Tahadhari


Inahitaji unyevu unyevu wakutosha wakati wakuweka kichwa.

Udhibiti magugu

Kabaji ina mizizi mifupi wakati wa kupalilia ni lazima kuwa mwangalifu usijerui mizizi yake. 

Unaweza tumia jembe la mkono kupalilia, ila ni vyema kutandaza nyasi kavu pembeni mwamiche (mulching) ya kabeji ili kuzuia magugu, 

 na pia kutunza unyevunyevu ambao ni muhimu wakati wote wa ukuwaji wa kabeji. 

Hasa wakati wa kuweka kichwa.

Mbinu muhimu za Kabeji

Mulching (kutandaza pembeni mwamiche)


Kutandazia pembeni mwamiche ni muhimu kwa kabeji. 

Kuna aina nyingi ya matandaza ambayo ya weza tumika kwa mfano randa za mbao, 

unga wa mbao unaopatikana wakati wa kuranda, 

pumba za mchele, majani makavu na nyingine nyingi. 

Utumia kuzuia magugu na kuhifadhi unyevunyevu.

Uvunaji

  • Kutegemeana na aina ya kabeji, kabeji ya weza kuwa tayari kuvunwa baada ya siku 60 mpaka siku 120 baada ya kutolewa kwenye kitaru.                                                    Kazi ya kuvuna hutakiwa kufanyika asubuhi or jioni sana.                                                                                      Kuvuna unaweza tumia mashine au mikono. Ufanyika kwa kukata chini ya kichwa cha kabeji kuelekea kwenye shina kwa kukadilia Sm 2 mpaka Sm 3;                   majani ya nje ya kichwa huondolewa na kuacha majini machache ya ndani kwa ajili ya kulinda kichwa.      Kuvuna kunatakiwa kufanyike kwa wakati kabila ijakomaa sana.
  • Kuchelewa kuvuna usababisha kurefuka kwa shina la kabeji, kupoteza ubora na vichwa kupasuka.

Mavuno

Kabeji uwezatoa tani 12 (kilo 12,000) mpaka tani 40 (kilo 40,000) kwa hekta.

Uhifadhi

Kabeji uweza hifadhiwa kwa muda mrefu, ikihifadhiwa kwenye mazingira ya baridi  na yenye hewa ya kutosha. 

Kati hali hii, kabeji huweza hifadhi kwa miezi miwili bila kupoteza ubora wake.


Kabeji huweza kuhifadhi kwa miezi katika mazingira ya kutengenezwa yenye RH ya 98% mpaka 100%, O2 ya 1%, CO2 YA 5% na nyuzi joto za 00c mpaka 10c.

Wadudu wa Haribifu


Nmb.
Jina
Matukio
Kudhibiti
1.
Diamond Back Moth

Utaga mayai chini ya majani, uharibu majani. Ula chini ya majani   nakuondoa rangi ya kijani na kuacha weupe. Huongoza kuharibu kilimo cha kabeji.
 Tumia viuatalifu, kwa mfano waweza tumia Deltamethrinkupulizia shamba.

2.
Cabbage Aphids

· Hufyonza maji na virutubisho toka kwenye mmea hasa chini ya majani. Hudhofisha mimea.
· Tumia viuatalifu, kwa mfano waweza tumia Acephate 25g/L kupulizia shamba.
3.
Cutworm

·        Uharibu mme mzima kwa kukata mche michanga kwenye shina karibu na udongo hasa wakati wa usiku
·    Handaa shamba mapema kwa kubalilia na kuondoa magugu kabisa shambani kabila ya kupanda kabeji shambani.
· Tumia viuatalifu, kwa mfano waweza tumia Carbaryl kupulizia shamba.

Magonjwa ya Kabeji





Nmb.
Jina
Matukio
Kudhibiti
1.
Damping-off

·   Madhara huonekana katika miche midogo usababishwa na Fangasi.
·Usambabisha kuchipua vibaya kwa mbegu na kufa kwa miche na kusababisha kupungua kwa miche shambani.
     Tumia mbegu zenye ubora.
     Epuka kumwagilizia maji juu ya miche mengi.

2.
Downy mildew

·  Ugonjwa huonekana kama vile unga sehemu za juu ya majani, shina, maua na hata kabeji.
Epuka kumwagilizia maji juu ya miche mengi.
  Tumia viuatalifu, kwa mfano waweza tumia Thiophanate Methyl kupulizia shamba.

3.
Black rot

·  Husababishwa   na bacteria
·      Tumia mbegu zenye ubora.
·     Epuka kumwagilizia maji juu ya miche mengi.

Comments

Popular posts from this blog

kilimo Cha Bamia