Kilimo Cha Kabeji
Aina ya Kabeji Kabeji inayokuwa mapema Kabeji inayokuwa taratibu Aina za Mbegu o Drumhead variety Ina vichwa vikubwa sana na mara nyingi ni bapa juu. Ipo katika aina za kabeji zinazo kuwa taratibu kwasababu inachukuwa siku 110 mpaka siku 120. Ikikuwa ina kichwa chenye uzito wa kilo 2 mpaka kilo 2.5. Upasuka kwa uwepesi. o Copenhagen Ina vichwa vya mviringo na ipo katika aina za kabeji zinazo kuwa mapema ikitumia siku 90 mpaka siku 100, ila upasuka kwa uwepesi. o Ox heart Huwa na vichwa vidogo vyenye umbile kama moyo. Ipo katika aina za kabeji zinazo kuwa mapema ikitumia siku 90 mpaka 100, haipasuki kwa uwepesi na inaradha nzuri. o Early Jersey Ina vichwa mfano wa koni vyenye ukubwa wa kati. Ipo katika aina za kabeji zinazo kuwa mapema ikitumia siku 90 mpaka 100. Zenye vichwa vyenye uzito wa kilo 1.5 mpaka kilo 2. o Glory of ...